Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kamwe amesema mchezaji huyo pamoja na wengine watatambulishwa baada ya taratibu za ndani kukamilika
"Mchezaji namba sita tayari amewasili nchini, tunapozungumza wakati huu mchezaji huyo yupo katika mikono salama ya Yanga. Hivyo mashabiki wakae tayari kumpokea mchezaji mkubwa"
"Tumeandaa utaratibu wa utambulisho wake pamoja na wenzake. Tulimtambulisha Nickson Kibabage kwa heshima ya mwaliko tuliopewa na Serikali ya Malawi, lakini upo utaratibu tuliandaa na tutautumia katika kutambulisha wachezaji wetu"
"Tunasubiri kocha wetu mkuu (Miguel Gamondi) awasili, tunatarajia atatua nchini Ijumaa (leo) na baada ya hapo tutatangaza benchi la ufundi"
"Kisha tutaanza kuwatambulisha wachezaji wapya akiwemo namba sita ambaye utambulisho wake tumeufanya kuwa wa mwisho," alisema Kamwe
Post a Comment