Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kamwe amesema namba sita atakuwa mchezaji wa mwisho kutambulishwa mapema wiki ijayo ambapo amebainisha kuwa utambulisho wake utaitikisa nchi
"Tutamtambulisha saa 6 na dakika 6 usiku, tunataka tukio hili liwe kama sherehe za maadhimisho ya Mwaka mpya"
"Baada ya utambulisho wake mashabiki wa Yanga wataingia mtaani kusherehekea ujio wa mchezaji huyu mkubwa lakini kuna wengine watahuzunika sana"
"Yaani siku hiyo kwa furaha ambayo Wananchi watapata, mafataki yatapigwa, ngoma zitapigwa, nyimbo zitaimbwa kila pande ya nchi hii watu watafurahi"
"Baada ya utambulisho wake, kesho yake asubuhi atakuwa hapa Makao Makuu ya CRDB ambao mashabiki wa Yanga watapata nafasi ya kuwa wa kwanza kupiga nae picha baada ya kujiunga kuwa Wanachama au kulipia kadi zao za uwanachama au shabiki," alisema Kamwe
Post a Comment