Musonda apewa tano Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Uongozi wa Yanga, umeweka wazi kuwa, mshambuliaji wao Kennedy Musonda ni mtu wa kazi kweli kutokana na uwezo alionao katika kasi ya kufunga mabao.


Nyota huyo kwa sasa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi raia wa Argentina ambaye amerithi mikoba ya Nasreddine Nabi.


Katika mchezo wa Wiki ya Mwananchi uliochezwa Jumamosi iliyopita Uwanja wa Mkapa, ubao uliposoma Yanga 1-0 Kaizer Chiefs, Musonda alipachika bao la ushindi dakika ya 45 akitumia pasi ya Maxi Nzengeli.


Akizungumza nasi, Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga alisema miongoni mwa washambuliaji wazuri waliopo kwenye kikosi cha Yanga ni pamoja na Musonda.


“Wengi wanapenda kuziweka kando rekodi lakini ukiangalia kwenye mchezo wetu dhidi ya Kaizer Chiefs Musonda alionesha kitu, yule ni mtu wa kazi ambaye anajua kutimiza majukumu yake.


“Mashuti matatu alipiga na katika hayo ni mawili yalikwenda nje ya lango, huku moja alilopiga likilenga lango na kuwa bao, hivyo anaonesha ana kitu.


“Alipokuja alibadilishiwa majukumu kwa kuwa alimkuta Fiston Mayele kwenye eneo hilo, hivyo nafasi yake ni eneo la ushambuliaji ataonesha uwezo wake kwa kufanya kazi kwenye eneo lake halisi,” alisema Kamwe.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post