Murtaza Mangungu atoa neno kauli ya Mo kukata tamaa

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, amevunja ukimya kuhusu ishu ya Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohammed Dewji 'Mo' 'ku-tweeti' kuwa amekata tamaa.


Mo alitwiti jana katika ukurasa wake wa Twitter kuwa 'mchakato wa uwekezaji unachelewa na yupo mbioni kukata tamaa' lakini hata hivyo ndani ya muda mfupi, ujumbe huo ulifutwa.


Aakizungumzia suala hilo mepama hii leo Julai 12, 2023 kupitia Kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM, Murtaza alisema hawezi kulizungumzia kwani ni binafsi.


“Mimi sio Msemaji wa Mo Dewji siwezi kuzungumzia mambo yake, Simba tunaendelea na tulichokusudia kama yeye ana maoni yake ni uhuru wake kuongea,” alisema Murtaza Mangungu.


Murtaza alisema, wao kama Simba hawana tatizo lolote na Mo kwani wameingia naye mkataba huku mchakato wa uwekezaji ukiendelea kwa mujibu wa sheria.


"Bilioni ishiri ipo na tunaendelea kuitumia kwani tuna mkataba, hata tulipomaliza uchaguzi aliteua wajumbe wa bodi na ni watendaji mpaka sasa hakuna tatizo lolote," alisema.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post