Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Winga wa zamani wa Yanga Saimon Msuva amesema usajili wa Nickson Kibabage utakuwa na manufaa kwa Yanga
Yanga imemsajili Kibabage kutoka klabu ya Singida Fountain Gate akisaini mkataba wa miaka miwili
Msuva amesema anamfahamu vizuri Kibabage kwa kuwa amewahi kucheza nae kunako klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco, ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja tena kwa ufasaha
"Nakumbuka wakati anarudi Tanzania watu walimbeza kama hivi, lakini nilijua atawashangaza"
"Nikawaona tena watu wakishangaa walipomuona akicheza kama winga badala ya beki kisha akafanya tena vizuri, hizo ni nafasi mbili ambazo anajua kuzicheza vizuri"
"Akiwa na Yanga atawashangaza zaidi muhimu wamwamini na kumpa nafasi, " alisema Msuva
Post a Comment