Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2022/23 pamoja na kombe la Shirikisho barani Afrika, anaweza kuibukia Misri kunako klabu ya Pyramids
Pyramids wamefikia mahitaji ya Yanga wakitajwa kuweka mezani dau la takribani Tsh Bil 2.8 pamoja na mshahara mnono kwa Mayele ambao ni mara mbili ya ule ambao Yanga walimuwekea ili kumuongezea mkataba
Mayele amebakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake, kama Yanga hautamuongezea mkataba au kumuuza sasa, msimu ujao ataondoka bure akiwa mchezaji huru
Mazingira haya yameiweka Yanga katika 'dilema' lakini ni wazi maamuzi ya mwisho lazima yazingatie maslahi kwa pande zote mbili
Kinachosubiriwa sasa ni taarifa rasmi kuhusu mshambuliaji huyo kuuzwa lakini muhimu zaidi shauku kubwa ya Wananchi itakuwa kumfahamu mshambuaji atakayetua kuchukua nafasi yake
Post a Comment