Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambuliaji kinara wa Yanga na mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita, Fiston Mayele amewashusha presha mashabiki wa klabu hiyo mara baada ya kuonekana akiwa amevalia jezi mpya ya Yanga kwa ajili ya msimu wa 2023/24 mara tu baada ya kuzinduliwa.
Mayele ambaye ni raia wa Congo DR akiwa na 'mamodo' wengine ameonekana katika tangazo la uzinduzi wa jezi hizo, illilopostiwa kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Yanga na kusambaa kwenye mitandao mingine ya kijamii.
Jezi za Yanga zimezinduliwa jana na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera wakati wa hafla fupi mara baada ya Yanga kuwasili nchini humo kufuatia mwaliko wa rais huyo kwenye sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa taifa la Malawi.
inafahamika kuwa, Mayele ambaye ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita na mfungaji bora wa michuano ya CAFCC amekuwa akiwindwa vilabu na vilabu vya Afrika kama Kaizer Chiefs pamoja na vilabu vya Uarabuni ambao wamemuwekea dau nono ili kupata huduma yake.
Lakini kwa upande wao viongpzi wa Yanga wamekuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha wanambakisha Mayele ambaye amesalia ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga ili Wananchi waendelee kutetema msimu ujao.
Hivyo baada ya Mayele kuonekana na jezi mpya, huenda mabosi hao wakiongozwa na Rais wao Eng. Hersi Said wamefanikiwa kumbakisha Mkongomani huyo.
Post a Comment