Mandonga achezea kichapo cha Wanyonyi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Aliyewahi kuwa mshindi wa Mkanda wa ABU, bondia wa Kenya, Daniel Wanyonyi amelipiza kisasi dhidi ya bondia wa Tanzania, Karim Mandonga kwa kumtwanga katika pambano lao lililofanyika siku ya jana katika Ukumbi wa Sarit Center jijini Nairobi, Kenya.


Hili lilikuwa pambano la marudiano ambapo katika pambano la kwanza lililofanyika Januari 14 mwaka huu nchini Kenya Karim Mandonga aliibuka mshindi mbele ya bondia huyo.


Pambano hilo la uzito wa light-heavy weight lisilokuwa la ubingwa, Wanyonyi alianza kutawala tangu raundi ya nne, huku akimwangusha mandonga mara mbili kwa konde nzito nzito lakini alijikaza mpaka kumaliza raundi 10.


Majaji watatu walitoa alama zao kwa Wanyonyi na Mandonga kama ifuatavyo, George Athumani 100-88, Wycliffe Marende 100-88 na Leonard Wanga 100-80, hivyo Wanyonyi kuibuka mshindi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post