Man United wachezea kichapo kwa Real Madrid

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Manchester United imepokea kipigo cha pili ndani ya saa 24 zilizopita baada kulala 2-0 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika dimba la NRG, Houston Marekani.


Jude Bellingham alifunga bao lake la kwanza ndani ya uzi wa Real Madrid mapema kipindi cha kwanza kabla ya Joselu kufungua akaunti yake mwishoni mwa kipindi cha pili.


Mabao yote ya Real Madrid yalikuwa ya aina yake huku licha ya kipigo nyanda Mcameroon, Andre Onana akiwa na mchezo mzuri golini kwa mara ya kwanza ndani ya uzi wa Man United. Manchester United imeendelea kudhihirisha kwanini ipo sokoni kutafuta mshambuliaji wa kati.


Hii ni mechi ya tano kwa Mashetani Wekundu katika mfululizo wa mechi za maandalizi ya msimu mpya kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Leeds United, ushindi wa 1-0 dhidi ya Lyon, ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal na kipigo cha 3-1 dhidi ya Wrexham AFC.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post