Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Real Madrid inatarajia kushuka dimbani usiku wa leo kukipiga na klabu ya Manchester United nchini Marekani katika mchezo wa kujiandaa na msimu ujao.
Mchezo kati ya Real Madrid na Man United ni moja ya michezo yenye mvuto zaidi duniani kwani ni timu ambazo zina mashabiki wengi zaidi ulimwenguni hivo wanapokutana mara nyingi mchezo unakua wenye mvuto mkubwa.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika jiji la Houston usiku wa leo ambapo vikosi vya timu zote tayari vimeshafika katika jiji hilo wakisubiria mtanange huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini humu na duniani kwa ujumla.
Timu hizo zimeshawahi kukutana nchini Marekani katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya kama huu mwaka 2014 na uliishia kuweka rekodi kubwa ya kujaza mashabiki kwani mchezo huo uliingiza mashabiki 109,318.
Vilabu vya Real Madrid na Man United ambavyo mara ya mwisho vilipokutana nchini Marekani viliweka rekodi ya kujaza mashabiki wengi katika mchezo huo, Lakini pia mwaka huu wamefanikiwa kumaliza tiketi mwanzoni mwa mwezi huu ambapo tiketi za mchezo zilikua zimeshamalizika.
Post a Comment