Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amesema serikali imedhamiria kufanya ukarabati mkubwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam ili kuufanya uwanja huo kuwa wa kisasa zaidi.
Yakubu amesema maboresho hayo yatafanyika katika maeneo ya kuchezea, vyumba vya wachezaji na kutoa viti vyote vya uwanja huo
Yakubu ametoa kauli hiyo leo Julai 27, 2023 Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kwa ajili ukarabati huo
Aidha Katibu Mkuu amesema uwanja huo utaendelea kutumika kama kawaida hadi pale ukarabati wa eneo la kuchezea utakapoanza.
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) liliagiza uwanja huo kufanyiwa maboresho baada ya ukaguzi uliofanyika mwezi May 2023
Uwanja huo unatarajiwa kutumika kwenye michuano ya African Footbal League ambapo klabu ya Simba kutoka Tanzania ni miongoni mwa timu nane zitakazoshiriki
Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007), Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha Tsh Bilioni 137
Post a Comment