Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Fred alikuwa nahodha wa SC Villa ambapo katika msimu uliopita alishinda tuzo ya beki bora wa msimu
Beki huyo pia amekuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda inayonolewa na Kocha Micho. Pia anamudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji
Beki kapanda hewani (wa kwanza kushoto pichani chini), mwili jumba! mwamba haswa katika kucheza mipira ya juu!
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa Yanga imemsajili Fred kuchukua nafasi ya Mamadou Doumbia ambaye tangu aliposajiliwa kwenye dirisha dogo msimu uliopita, hakuweza kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Huu unaweza kuwa usajili wa 'surprise' kwani tayari Yanga ilishatangaza kukamilisha usajili wake
Wananchi wanasubiri utambulisho wa wachezaji wao wapya ambapo Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wakati wowote wanaanza kushusha 'vyuma'
Post a Comment