Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Chelsea ina mpango wa kumsajili Neymar katika dirisha hili la usajili barani Ulaya iwapo PSG itakubali kumuuza kwa kiasi cha pesa ambacho kitakuwa pungufu ya Euro 100 milioni.
Neymar amekuwa akihusishwa kuondoka PSG kwa sababu hana furaha, na pia ni mpango wa matajiri hao wa Jiji la Paris kutaka kupunguza matumizi katika kikosi chao hususan yale ya ulipaji mishahara.
Kocha mpya wa Chelsea, Mauricio Pochettino ndiye anadaiwa kupendekeza jina la nyota huyu kwani alishawahi kufanya naye kazi kwenye kikosi cha PSG.
Mbali ya Pochettino inaelezwa kuwa beki wa Chelsea, Thiago Silva ambaye ana ukaribu na Neymar kama mshkaji wake anahusika kwenye mpango wa ushawishi kwa staa huyu akubali ofa ya kutua kwenye viunga hivyo vya Darajani
Post a Comment