Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Tabora United (zamani Kitayose FC imetangaza kumsajili Mlinda mlango John Noble (30) raia wa Nigeria kutoka klabu ya Enyimba ya Nigeria.
Noble ameanguka saini ya mkataba wa mwaka mmoja wa kuwatumikia Nyuki wakali hao wa Tabora mpaka 2024.
Hata hivyo inaelezwa klabu ya Simba iliingilia kati dili hilo Kwa ajili ya saini ya nyanda huyo kuziba pengo la Jefferson Luis raia wa Brazil ambaye amepata majeraha na hayupo kwenye mipango ya Wekundu hao wa Msimbazi.
Hata hivyo mipango ya Wekundu hao wa Msimbazi imekwama, Noble ni mali ya Tabora United.
Noble alikuwa nahodha wa Enyimba na pia kujumuishwa kwenye kikosi cha Nigeria kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka nchini Cameroon mwaka jana.
Post a Comment