Kikosi hiki wote kuanzia leo hawana ajira - EDUSPORTSTZ

Latest

Kikosi hiki wote kuanzia leo hawana ajira

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kumekucha huko kwenye dirisha la usajili wa mastaa wa soka duniani, ambapo wamekuwa bize kubadili timu kutoka moja kwenda nyingine wakati huu wakijiandaa na msimu mpya wa 2023-24.


Tangu Januari, klabu zimekuwa na uhuru wa kufikia makubaliano na wachezaji ambao mikataba yao itafika tamati mwisho wa msimu, lakini kuna wengine bado hawajabamba dili hizo na hivyo watakuwa hawana ajira kuanzia leo Jumamosi.


Na kwenye orodha hiyo ya mastaa ambao watakuwa hawana ajira kuanzia leo Jumamosi wapo mastaa wenye majina makubwa kwelikweli ambao ungehitaji kuwaona kwenye timu yako.


Hiki hapa kikosi kizima cha mastaa ambao wataanza Jumamosi ya leo, Julai Mosi wakiwa hawana ajira. Wape dili.


Kipa - David de Gea


Baada ya miaka 12 ya kuitumikia Manchester United, kipa David De Gea hatimaye atakuwa huru kuachana na timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika na imu yake imeondoa dili la kumpa mkataba mpya.


De Gea, 32, alikuwa akilipwa Pauni 375,000 kwa wiki huko Old Trafford, lakini kocha Erik ten Hag anahitaji kipa mwenye uwezo wa kuucheza mpira kwa miguu, jambo ambalo ni mtihani mzito kwa Mhispaniola huyo. Baada ya kuwa huru na kama Man United na De Gea watakuwa wameshindwana, kipa huyo hawezi kukosa timu za kwenda kujiunga nazo.


Beki wa kulia - Matt Doherty


Baada ya kutumikia miezi sita iliyopita kwa mkopo huko Atletico Madrid akitokea Tottenham Hotspur, Matt Doherty sasa anafikiria mahali gani pa kwenda baada ya kushindwa kuwashawishi Wahispaniola hao ambao walimtumia kwenye mechi mbili tu.


Kwa umri wake wa miaka 31, staa huyo wa kimataifa wa Ireland, bado ana uhamisho mmoja mkubwa anaoweza kufanya kwenye maisha yake ya soka na huenda akapata nafasi ya kujiunga na moja ya timu kwenye Ligi Kuu England kutokana na uzoefu wake.


Beki wa kati - Milan Skriniar


Bila shaka atakuwa nahodha wa timu hiyo, Milan Skriniar, 28, alikuwa na msimu mgumu huko Inter Milan kutokana na kusumbuliwa a majeruhi, lakini anaendelea kuwa mmoja wa mabeki wa kati bora kabisa Ulaya kwa sasa.


Ishu ya kuhamia PSG ilitajwa sana, lakini hakuna kilichothibitishwa na jambo hilo linaweza kumfanya anaswe na timu za Ligi Kuu England, hasa Manchester United ambao walijaribu kuwasiliana naye kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Rekodi yake ya kuumia mara kwa mara ndicho kitu kinachotia mashaka.


Beki wa kati - Caglar Soyuncu Alitazamwa kama beki anayekuja kwa kasi kwenye soka la dunia baada ya msimu wake wa kwanza tu Leicester City, kabla ya maisha ya mkali huyo wa kimataifa wa Uturuki, Caglar Soyuncu kutibuka kwa siku za karibuni.


Haonekani kama atapata nafasi ya kujiunga na timu na timu nyingine ndani ya Ligi Kuu England kutokana na kiwango chake cha msimu uliopita, lakini kuna timu nyingi za ng'ambo zimekuwa zikihitaji saini ya beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 27, hasa Atletico Madrid wamekuwa wakihusishwa naye kwa karibu.


Beki wa kushoto - Daley Blind


Baada ya kutumikia muda wake huko Bayern Munich msimu uliopita, Daley Blind sasa yupo kwenye msako wa klabu mpya kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi akiwa na umri wa miaka 33.


Nguvu ndicho kitu kinachomtatiza Mdachi huyo, udhaifu ambao amekuwa akiuficha kwa ujuzi wake wa soka la kutumia akili nyingi. Ilielezwa kwamba alizungumza na kocha wake wa zamani wa huko Ajax, Erik ten Hag ili arudi kuitumikia Manchester United anakofanya kazi kocha huyo kwa sasa.


Kiungo wa kati - Alex Oxlade-Chamberlain Staa mwingine wa maana aliyeachana na Liverpool kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kutokana na mkataba wake kumalizika. Oxlade-Chamberlain amekuwa akisumbuliwa sana na majeruhi kwa siku za karibuni.


Wakati akianza siku ya leo Julai Mosi akiwa si mwaajiri wa timu yoyote, staa huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kukipiga huko Saudi Arabia, ambako wapo siriazi kwenye ishu ya kufanya usajili wa wachezaji wenye majina makubwa katika dirisha hili.


Kiungo wa kati - Angel Di Maria


Akiwa amejiunga na Juventus kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana. Kiwango chake alichokwenda kukionyesha kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 akiwa na kikosi cha Argentina kilionyesha bayana ubora wa staa huyo aliposaidia timu yake kubeba ubingwa wa kombe hilo.


Kiwango chake alichoonyesha alipokuwa England kwenye kikosi cha Manchester United kinafifisha uwezekano wa staa huyu kurudi kwenye Ligi Kuu England. Umri wake ni miaka 35, lakini bado miguu yake ina kitu kikubwa inachoweza kukifanya ndani ya uwanja.


Kiungo mshambuliaji - Daichi Kamada


Aliliweka jina lake matawi ya juu wakati anakipiga Eintracht Frankfurt ambapo alikuwamo kwenye kikosi kilichonyakua ubingwa wa Europa League mwaka 2022. Mjapani huyo, Daichi Kamada yupo huru kuhama timu hiyo kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kutokana na mkataba wake kufika mwisho.


Kuna timu kibao zinahitaji saini yake, na huenda akaibukia kwenye Ligi Kuu England kwa sababu huduma yake si hapa, ambapo kwenye Bundesliga kwa msimu uliopita alifunga mabao tisa.


Winga wa kulia - Marco Asensio


Staa wa kiwango cha dunia anapokuwa kwenye ubora wake. Marco Asensio ni mshindi mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ataachana na Real Madrid kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi kutokana na mkataba wake kufika tamati.


Winga huyo anayetumikia mguu wa kushoto ana uwezo pia wa kucheza kiungo ya kati, huku saini yake ikivutia timu nyingi ikiwamo mabingwa wa Ufaransa, PSG. Uhamisho wa kuhamia kwenye Ligi Kuu England unapewa nafasi kubwa ya kutokea kutokana na timu za Chelsea na Aston Villa zote kuhitaji saini yake.


Mshambuliaji wa kati - Roberto Firmino


Moja ya wachezaji bora kabisa waliopata kutokea kwenye kikosi cha Liverpool kwa miaka ya karibuni. Roberto Firmino ataachana na maisha ya Anfield kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa na uzoefu mkubwa kitu ambacho kitavutia timu nyingi za nje ya Ligi Kuu England. Staa huyo wa kimataifa wa Brazil kwa siku za karibuni amekuw akihusishwa na mpango wa kwenda kukipiga huko Saudi Arabia.


Wingi wa kushoto - Wilfried Zaha


Staa mwingine kwenye viwango bora kabisa kwenye soka la kisasa, ambaye ataachana na timu yake kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, ilielezwa kwamba ameshapewa ofa ya dili jipya la kubaki kwenye timu hiyo, lakini kilichothibitishwa.


Uhamisho wa kwenda Saudi Arabia unaripotiwa kuwa kwenye mpango na kinachosubiriwa kama dili hilo litatiki wakati mchezaji huyo akiwa huru kuanzia leo Jumamosi.Zaha mwenyewe anahitaji kujiunga na timu itakayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Chanzo: Mwanaspoti



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz