Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wiki hii Yanga itafunga hesabu zake za usajili kwani dirisha la usajili kwa michuano ya CAF litafungwa Jumatatu ijayo
Baada ya Fiston Mayele kuuzwa, Wananchi wanasubiri kwa hamu ujio wa mshambuliaji atakayechukua nafasi yake
Usajili wa mshambuliaji huyo imeelezwa uko katika hatua za mwisho, Wananchi wakae tayari kumpokea
Hapa tunamzungumzia mfungaji bora wa ligi kuu ya Cameroon 2022/23 Emmanuel Dikongue Mahop kutoka klabu ya Cannon Younde akimaliza msimu na mabao 15, assist 3
Kwa kuzingatia mahitaji ya Yanga msimu ujao, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amepambana kwelikweli kuinasa saini ya mshambuliaji huyo ambaye timu nyingi zimehitaji huduma yake
Mahop ana kasi, nguvu na maarifa ya kuwatoka mabeki. Anatumia vyema miguu yake yote miwili akiwa miongoni mwa washambuliaji wa timu ya Taifa ya Cameroon (sio ile ya CHAN)
Kabla ya kutua Cannone Younde, Mahop aliitumikia Fc Akonagui ambapo katika msimu wa 2019/20 alipachika mabao 24 na kutoa assist 5
Huyu ni mchezaji sahihi kuvaa viatu vya Mayele anayesubiri kutangazwa na klabu ya Pyramids Fc ya Misri
Post a Comment