Huyu hapa Kocha wa Yanga aliyeondoka na timu kwenda Malawi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa kikosi cha timu hiyo kilichoondoka nchini kwenda Malawi kipo chini ya kocha wa Under 20, Said Maulid baada ya kocha msaidizi wa timu hiyo, Cedric Kaze kuwa mapuzikoni huku pia Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi akiwa hajawasili nchini.


Hersi amesema hayo leo wakati kikosi cha timu hiyo kikiondoka kwenda Malawi kwenye mchezo wa kirafiki na Nyasa Big Bullets wakati wa sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Taifa hilo zitakazofanyika kesho.


“Timu iliyoenda Malawi kuna mchanganyiko wa timu kubwa na Under 20, kwa hiyo benchi la ufundi lipo chini ya mwalimu wa Under 20, Said Maulid (SMG), pia kuna mchanganyiko wa viongozi kutoka timu kubwa ambao wameambatana na timu,” amesema Hersi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post