Hivi hapa Viingilio SIMBA DAY

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally ametangaza viingilio vya Tamasha la Simba Day litakalofanyika August 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ahmed amesema Simba inawahitaji mashabiki wake uwanjani kwa wingi kuliko fedha hivyo wameweka viingilio rafiki ili kila Mwanasimba aweze kumudu

"Kwa upande wa viingilio, sisi kama klabu tunahitaji fedha lakini kwenye tamasha tunahitaji zaidi mashabiki, Wanasimba waje zaidi ndio maana tunawatafuta wadhamini kama CRDB ili walete fedha. Tunajali zaidi maslahi ya Wanasimba"

"Viingilio vya Simba Day ni Platinum – Tsh. 200,000, VIP A – Tsh. 40,000, VIP B – Tsh. 30,000, VIP C – Tsh. 20,000, Machungwa – Tsh. 10,000 na Mzunguko – Tsh. 5,000"

"Kispika kinarudi mtaani kuwaita Wanasimba kwenye Simba Day. Tunaenda kuwaonyesha kwamba Uwanja wa Mkapa ni mdogo sana kwa Simba kuujaza"

"Waliopandisha kibegi kwenye Mlima Kilimanajaro, watu wote tisa tutawaalika kwenye Simba Day na watapata nafasi ya kutambuliwa na mashabiki kwenye siku ya tamasha letu"

"Kikosi kitarejea kutoka Uturuki tarehe 1 ya mwezi Agosti," alisema Ahmed

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post