Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ahmed amesema katika misimu sita iliyopita, Simba imetangaza Utalii Tanzania kupitai Visit Tanzania, huu ni wajibu kwa klabu kutangaza utalii wa Tanzania
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed ameandika ujumbe huu;
"Wengi wanadhani tumeamua kuzindua jezi Juu ya Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kujibu mapigo ya wale waliogawa jezi Lilongwe"
"Kwa miaka sita sasa tumekua tukibeba bendera ya utalii wa nchi kupitia Visit Tanzania. Sisi tunaamini tunaowajibu wa kuisaidia Serikali yetu kutangaza Utalii wetu"
"Tangu tumetangaza kuzindua jezi juu ya Mlima Kilimanjaro, taarifa imesambaa dunia nzima na kila mmoja anahamu ya kushuhudia tukio hilo Kuzindua Jezi juu ya Mlima"
"Ni tukio la kwanza duniani, hivyo dunia nzima inasubiri kushuhudia itakuaje Wakati wanashuhudia uzinduzi wa jezi, hapo hapo wanaushuhidia uzuri wa Mlima Kilimanjaro"
"Tukio litakua Mubashara kupitia channel zote za Simba hivyo watu watakiona kilele cha Mlima Kilimanjaro. Tunaamini kwa tukio hili wengi watavutiwa na kuhamasika kupanda Mlima Kilimanjaro Na hapo Simba tutakua tumetimiza malengo yetu," aliandika Ahmed
Post a Comment