Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Katika vikao vya timu hiyo vilivyofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam chini ya Rais wa klabu hiyo itakayofahamika kama Singida Fountain Gate, Japhet Makau viliazimia kuingia moja kwa moja ili kuwapata nyota hao wanaoamini watakuwa na mchango mkubwa katika michuano itkayoshiriki hasa ya CAF.
Singida ni moja ya timu nne zitakazoiwakilisha nchi kwenye michuano ya CAF msimu ujao utakaoanza mwezi ujao na vikao hivyo vilikuwa vikijadili mammbo kadhaa ikiwamo ishu za usajili na
chanzo kutoka ndani ya timu hiyo kililiambia Mwanaspoti, licha ya ukubwa wa Simba na Yanga Ila viongozi wa Singida wameamua kuingia kati dili hizo kutokana na wachezaji hao kutaka kuondoka.
"Unaposhiriki kwenye mashindano makubwa kama ya Afrika ni lazima ushindanie wachezaji na wapinzani wako ndio maana hatujaogopa kubisha hodi kwa Simba na Yanga," kilisema chanzo chetu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Singida, Olebile Sikwane aliliambia Mwanaspoti katika vikao hivyo kulikuwa na mambo mengi yaliyokuwa yanajadiliwa ila lengo likiwa ni kutengeneza timu imara kwa msimu ujao.
"Tumekuwa na vikao vya muda mrefu lakini vyenye tija kwa sababu kama unavyojua msimu ujao tunashiriki michuano mingi na mikubwa hivyo ni lazima tujipange vizuri," alisema.
Aidha Sikwane alisema mbali na kujadili mambo ya usajili ila pia walikuwa wanajadili kuhusu mustakabali wa Kocha Mkuu, Hans Pluijm ambaye mkataba wake umemalizika tangu juzi Juni 30.
"Hadi Julai 10 kila kitu tutakiweka wazi kuanzia safari yetu ya Tunisia kwenye maandalizi ya msimu mpya 'Pre- Season' na mambo mengine hivyo mashabiki zetu wawe na subra tu."
Onyango anadaiwa kuandika barua kwa mara ya pili kwa mabosi wa Simba ili aondoke kutafuta changamoto sehemu nyingine kutokana na ofa nzuri aliyowekewa na Singida sawa na Bangala ambaye naye katika mahojiano yake aliweka wazi ana asilimia 80 za kuondoka huku 20 tu zikiwa ni za kubaki kwenye kikosi cha Yanga.
Chanzo: Mwanaspoti
Post a Comment