Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amemuombea kipa namba moja wa Simba SC na Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' apone haraka kwani bado anahitajika dimbani.
Manara ambaye amefungiwa na TFF kujihusisha na masuala ya soka, amesema ni raha kwa Yanga kumfunga mpinzani wao Simba wakati langoni akidaka Manula badala ya Mbrazil Jefferson Luis ambaye anatajwa kuachana na klabu hiyo siku chache baada ya kusajiliwa kwa kinachoelezwa kuwa ni majeraha.
"Hakuna shaka yoyote Aishi Manula ni moja ya makipa hodari kuwahi kutokea Tanzania na anabaki kuwa golikipa namba moja nchini.
"Kwa sasa akiwa mapumzikoni akijiuguza niwaombe kwa sekunde japo moja kimoyo moyo tumuombee apone haraka ili tuje kumtungua yeye.
"Yes ni yeye pekee mwenye hadhi ya kufungwa na Young Africans, sio yule muuza matikiti wa Kibrazil, tungemuonea sana.
"Raha ya kuwafunga Makolo kipa awe Aishi bhana, pona haraka mwana tukuletee Aziz KI wako," amesema Manara.
Manula kwa sasa yupo katika kipindi hichi cha mapumziko akiendelea kujiuguza jeraha lake na kufanya mazoezi mepesi baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.
Post a Comment