Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Imefahamika kuwa uongozi wa Klabu ya Simba umepanga kumtambulisha kiungo wao mpya kutoka DR Congo, Fabrice Luamba Ngoma kama mchezaji wa mwisho kutokana na kuamini kuwa ndio usajili ambao utatikisa zaidi msimu huu.
Ngoma anaripotiwa kuvunja mkataba wake na Al Hilal Omdurman ya Sudan kutokana na ligi kusimama kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo, lakini hata hivyo klabu hiyo imekuja juu ikidai hajafuata kanuni zinazotakiwa, hivyo Simba SC wameenda kumalizana kistaarabu ili imbibe mwamba huyu.
Chanzo cha ndani ya Simba SC kimeelelza: “Simba SC imekamilisha taratibu zote za usajili wao hivyo kilichobaki kwa sasa ni utambulisho wa wachezaji ambao bado hawajatambulishwa.
“Ukiangalia mipango ya uongozi ni kuhakikisha kuwa wanamtambulisha Fabrice Ngoma mwishoni na ndio maana utaona tayari kuna wachezaji wametambulishwa mapema lakini Ngoma bado hajatambulishwa.
“Hiyo ni mipango ambayo wanaona kuwa Ngoma akitambulishwa mwishoni litakuwa jambo kubwa kwa kuwa ni usajili ambao uliimbwa sana kutokana na klabu hiyo kuhusiswa na kuwapokonya Young Africans mchezaji huyo,” kimeeleza chanzo hicho
Kwa upandea Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally yeye amesema:
“Simba SC msimu huu kila usajili ni usajili mkubwa na hakuna sijui usajili huu wa kawaida wala ule mkubwa kuliko huu, kila usajili utakuwa tishio jambo ambalo wanasimba wanatakiwa kulifanya ni kuendelea kuwa karibu na sisi kwani tutashusha vyuma vya maana.
Post a Comment