Eymael athibitisha kulipwa na Yanga

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa klabu ya Yanga imefunga kusajili kutokana na deni wanalodaiwa na aliyekuwa Kocha wao Luc Eymael, Yanga imemlipa kocha huyo


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alikiri kuchelewa kwa malipo ya awamu ya mwisho ambayo sasa wameshakamilisha, Luc amethibitisha kuwa amelipwa


"Robo tatu ya pesa wanazotakiwa kunilipa wamenipa, nashukuru kwa hilo kwa sababu nataka tumalizane kwa amani"


"Naipenda Tanzania kwani nilikuwa na wakat mzuri hapo, ni vile tu kulitokea changamoto, inabidi maisha mengine yaendelee," alisema


Yanga ilifikia makubaliano ya kumlipa Eymael kwa awamu, baada ya kuvunja mkataba wake kutokana na kauli za kibaguzi


Kocha huyo alifukuzwa nchini mwaka 2021 huku akipigwa marufuku kufundisha soka nchini Tanzania


Afrika Kusini pia ilimzuia Eymael kufanya kazi katika nchi hiyo kutokana na matamshi yake ya kibaguzi

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post