Baada ya kufanya mazoezi kwa siku chache na wenzake katika pre-season huko Uturuki, Chama amekiri kuwa timu imekuwa imara zaidi
"Tupo kwenye maandalizi ya msimu mpya kuna wachezaji wengi wapya tunapambana kuhakikisha tunatengeneza muunganiko mzuri ambao utakuwa na tija ndani ya timu msimu ujao"
"Lengo ni kuhakikisha tunamaliza msimu tukiwa na mataji muhimu ambayo yataturejesha kwenye ushindani hasa kimataifa ambapo tunatamani kuvuka hatua ambazo tayari tumezipiga kwa misimu minne mfululizo hilo linawezekana tukiendeleza juhudi zetu na kuwa wamoja," Chama aliongeza
"Timu yetu imeimarika, wachezaji wote waliosajiliwa ni wazuri, nafikiri tutakuwa na nyakati nzuri sana msimu ujao," alisema Chama
Chama alitua Uturuki Alhamisi iliyopita akiwa na Fabrice Ngoma na moja kwa moja kuanza mazoezi na wenzao waliotangulia
Post a Comment