Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Katika misimu ya nyuma ilizoeleka timu 16 zilizotolewa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa zilipewa nafasi ya kucheza mtoano kombe la Shirikisho ili kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho
Kuanzia michuano inayofuata, timu zitakazotolewa raundi ya kwanza ya ligi ya mabingwa zitaondoshwa mashindanoni kwani hakuna tena nafasi ya kupelekwa kucheza Shirikisho
Hivyo timu 16 zitakazofuzu raundi ya pili ya Shirikisho, zitatinga moja kwa moja hatua ya makundi
Kwa maana rahisi ni kuwa timu zitakazocheza ligi ya mabingwa hazitakuwa na nafasi ya kucheza kombe la Shirikisho katika msimu huo
Na zile zinazocheza Shirikisho tangu mwanzo ndizo zitakazokutana katika hatua ya makundi
Post a Comment