Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Sio tetesi tena, Yanga imemshusha mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast (2022/23) Pacome Zouzoua (MVP)
Pacome ni kiungo mshambuliaji ambaye pia anaweza kutumika katika eneo la kiungo cha ulinzi. Ndiye mchezaji bora wa mwaka wa Asec Mimosas pia
Katika msimu uliopita Pacome alifunga mabao saba na kutoa pasi nne za mabao.
Baada ya Yanga kumsajili Stephane Aziz Ki ambaye pia alitua Yanga akiwa MVP wa ligi ya Ivory Coast, Pacome alikabidhiwa majukumu ya kuibeba Asec Mimosas
Ametoa mchango mkubwa kwa kikosi cha Asec kilichotwaa ubingwa wa Ligi 1 ya Ivory Coast kwa msimu wa pili mfululizo pamoja na kutwaa taji la FA pia
Pacome pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Asec kilichofanikiwa kucheza nusu fainali ya kombe la Shirikisho katika msimu uliomalizika
Post a Comment