BREAKING: Simba wamtambulisha Fabrice Ngoma


Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza 
HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Hatimaye Klabu ya Simba imemtambulisha, Fabrice Luamba Ngoma aliyekuwa akihusishwa na timu hiyo kwenye kipindi hiki cha usajili.


Ngoma anayecheza nafasi ya kiungo ni mkabaji, inaelezwa juzikati umafia ulifanyika Airport usiku wa manane kwa kupitishwa mlango wa uwani na kujikuta Unyamani huku majirani wakiachwa hawaamini macho yao.


N0. 6 hiyo ya mpira raia wa Congo mwenye umri wa miaka 29 inadaiwa alifika Julius Nyerere International Airport kupitia Ndege ya Ethiopian Airline usiku huo lakini ‘Makomando’ wa Lunyasi wakafanya kazi yao na kuwaacha baadhi ya viongozi wa majirani waliojitokeza kwa shangwe na bashasha wapigwe na baridi huku wasijue cha kufanya.


Ngoma anakwenda kuimarisha eneo la kiungo, eneo ambalo Simba ilikuwa ikimtumia zaidi Sadio Kanoute na mara kadhaa Jonas Mkude ambaye ametimkia Yanga kwa sasa.


Simba ilikuwa ikipata wakati mgumu sana pindi Kanoute anapokosekana kikosini kwa changamoto ya kadi au ugonjwa, pengo lake lilikuwa likionekana waziwazi.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post