Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Bangala ambaye pamoja na Mkongoman mwenzie Djuma Shaban hawako kwenye mipango ya Yanga msimu huu kiasi hawakuwa sehemu ya utambulisho wa wachezaji waliotambulishwa kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi kilichofanyika tarehe 22.Julai. 2023.
Habari za uhakika kutoka kwenye chanzo cha kuaminika kinasema Yanga watapokea Tshs100M kwa biashara hii.
Bangala na Djuma wameigomea Yanga kwenda kwa mkopo Singida Fontain Gate baada ya kutokea mgogoro wa kimkataba na nafasi zao kuzibwa na Yao Yao na Pacome.
Azam itaondoa mchezaji mmoja wa kimataifa ili kumpa Bangala nafasi huku Azam wakitakiwa kumaliza biashara hii haraka.
Hapo awali baada ya fainali ya FA Cup kule Tanga, Bangala alionyesha nia kujiunga Azam kwa kuongea na viongozi wao huku kocha wa Azam pia akionyesha kumhitaji. Lakini dili halikufanyika baada ya Yanga kuwaomba Azam kuachana na biashara ya Bangala kwa kuwa walishawapa Feisal.
Post a Comment