Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Pamoja na kuwa 'Thank You' zao hazikutangazwa, ni wazi Yanga imeachana rasmi na wachezaji Yannick Bangala, Djuma Shabani, Mamadou Doumbia na Fiston Mayele
Suala la Mayele liko wazi kwani hata huko anakoelekea kunafahamika, Bangala na Djuma walirejea kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya lakini ni wazi uongozi umewaruhusu wakatafute changamoto sehemu nyingine kama ilivyo kwa Doumbia ambaye 'hakuwaka' mapema
Kundoka kwa wachezaji hao hakutaacha 'pengo' kwa Yanga kwani uongozi umetumia vyema dirisha la usajili kuziba nafasi zao
Yao Yao, amechukua nafasi ya Djuma, wakati Jonas Mkude amechukua nafasi ya Bangala huku Gift Fred akichukua nafasi ya Doumbia
Mbadala wa Mayele anasubiri kutangazwa lakini wakati huohuo Kennedy Musonda anaendeleza pale alipoishia
Post a Comment