Baleke, Onana, Malone waondoka kuelekea Uturuki Chama aendelea kuwagomea simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Baleke, Onana, Malone waondoka kuelekea Uturuki Chama aendelea kuwagomea simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wachezaji wanne wa kigeni wanatarajia kuungana na kikosi cha Simba nchini Uturuki baada ya taratibu zao za vibali kukamilika


Taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo, imebainisha kuwa wachezaji Che Fondoh Malone, Willy Essomba Onana na Jean Baleke wameondoka nchini leo ambapo watatua Uturuki hapo kesho


Aidha winga Aubin Kramo yeye ataungana wenzake mchana wa leo akitokea kwao Ivory Coast wakati kiungo Fabrice Ngoma anakamilisha vibali vyake kabla ya kuanza safari kuelekea Uturuki


Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema kiungo Clatous Chama sio miongoni mwa wachezaji waliosafiri suala lake likiwa bado linashughulikiwa na uongozi


Wachezaji wengine wanaendelea na mazoezi huko Uturuki leo ikiwa ni siku ya tano



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz