Bado wanne wanasubiri kutambulishwa - Kamwe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wiki hii wanakamilisha utambulisho wa wachezaji wanne


Katika mahojiano na Uhai Fm jana, Kamwe alisema baada ya kutambulisha wachezaji wa safu ya ulinzi na kiungo sasa wanahamia kwenye eneo la ushambuliaji


Katika wachezaji wanne, mmoja ni wa ndani na watatu wanatoka nje ya nchi akiwemo yule namba sita ambaye utambulisho wake utakuwa wa mwisho


"Tulianza kutambulisha safu ya ulinzi tukaja eneo la kiungo na winga sasa tumehamia eneo la kiungo wa ushambuliaji na washambuliaji"


"Tuna wachezaji wanne, mmoja ni wa ndani na watatu ni wa kigeni," alisema Kamwe


Katika hatua nyingine, Kamwe alieleza kushangazwa na wale wanaodhani timu kumuuza mchezaji ni kushindwa


Akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazomuhusu mshambuliaji Fistoni Mayele, Kamwe alisema kuuza wachezaji ni moja ya vyanzo vya mapato ya klabu


"Ni bahati mbaya hapa Tanzania timu ikiuza mchezaji nje inaonekana imeshindwa. Katika vyanzo vya mapato ya klabu, mauzo ya mchezaji ni moja ya chanzo kikubwa"


"Zipo sababu ambazo zinapelekea timu kumuuza mchezaji wake muhimu. Timu inaweza kupata ofa nzuri ambayo ina manufaa kwa klabu lakini pia kwa mchezaji mwenyewe anaweza kuondoka kwenda kutafuta changamoto nyingine kutokana na maslahi au mapenzi yake"


"Mchezaji akiwa na mkataba na timu moja sio kama amefungwa jela hawezi kuondoka, jambo muhimu ni makubaliano tu kwenye utaratibu wa kuondoka," alisema


Yanga inatajwa kumuuza Mayele baada ya kupokea ofa nono (Bil 2.8) kutoka klabu ya Pyramids


Miongoni mwa wachezaji wanne wanaosubiri kutambulishwa, wawili wanaweza kuwa washambuliaji kwa ajili ya kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji


Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Ivory Coast msimu uliopita, Sankara Karamoko huenda akatua kwa Wananchi


Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, anatokea klabu ya Asec Mimosas


Yanga pia inahusishwa na kinara wa mabao ligi kuu ya Zambia msimu uliopita Andy Boyeli wa Power Dynamos timu aliyokuwa akicheza Kennedy Musonda


Baada ya Musonda kujiunga na Yanga, Boyel aliiongoza Power Dynamo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zambia akifunga mabao 14


Pia yumo Sudi Abdallah raia wa Burundi mwenye umri wa 23. Msimu uliopita Sudi alicheza Ligi Kuu Bangladesh, kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika


Ni mshambuliaji ambaye pia huitumikia timu ya Taifa ya Burundi. Alikuwemo kwenye kikosi cha Burundi kilichocheza na Cameroon katika uwanja wa Benjamin Mkapa mwezi uliopita katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post