Azam FC wasusia mechi Tunisia mchezaji wao akivunjwa mkono

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mchezo wa kirafiki kati ya Wanalambalamba, Azam FC dhidi ya miamba ya Tunisia, Stade Tunisie uliokuwa ukichezwa nchini Tunisia umeshindwa kuendelea huku Waoka Mikate hao wakiwa nyuma 3-1.


Kwenye mchezo huo wa Kirafiki imeshuhudiwa Azam FC wakisusia mechi mara baada ya mwamuzi wa mchezo kuruhusu goli la nne la Stade Tunisien ambapo Kocha wa Azam hakuridhia maamuzi ya Mwamuzi na baadae kuwaamuru wachezaji wake watoke nje (Wagomee mechi) ikiwa ni dakika ya 60 ya Mchezo.


Akifafanua sababu za mchezo huo kushindwa kuendelea, Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem lbwe amesema sababu ni maamuzi ya Mwamuzi kutokuwa rafiki pamoja na wachezaji wa timu pinzani kutocheza kiungwana.


Ibwe amesema kutokana na mchezo huo kutokuwa wa kiungwana, beki wao Edward Charles Manyama amepata majeraha ya kuvunjika mkono wakati wa mchezo huo.


"Ni kutokana na maamuzi ya refaree haujawa mchezo wa kirafiki...mchezaji wetu amevunjika mkono," amesema Ibwe.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post