Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, saa 1 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi amesema ni siku kubwa kwa mashabiki wa Yanga kuukaribisha msimu mpya
Amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea msimu mpya wenye malengo makubwa
"Kesho ni siku kubwa kwa Mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania Klabu hii kubwa yenye historia kubwa"
"Kwenye upande wa timu bado tuko kwenye maandalizi, na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs tutautumia kama sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu ujao"
"Tunatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwasababu hii ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka Klabu hii iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa," alisema Gamondi
Post a Comment