Ahmed Ally awalipua Yanga sakata la Chama "subiri I miaka 13 ipite kwanza"

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Klabu ya Simba imesema kuwa wanaomtaka kiungo mshambuliaji wao, Clatous Chota Chama watasubiri sana kwani bado ana mkataba na klabu hiyo na wala haina mpango wa kumuuza.


Hayo yamesemwa na Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally wakati akifafanua kuhusu sakata la Chama ambaye anadaiwa kugoma kwenda Uturuki kwenye kambi na wenzake huku sababu ikitajwa kuwa ni kutaka kuboreshewa maslahi vinginevyo aondoke klabuni hapo.


"Hakuna changamoto yoyote ya kimkataba kati ya Chama na Simba, uzuri mikataba yote inakuwa sehemu tatu [nakala kwa mchezaji, klabu na TFF] kwa hiyo hakuna sintofamu yoyote ya mkataba.


"Chama ni miongoni mwa very professional players ambao tumewahi kuwanao, ni mchezaji ambaye huwa anasoma mkataba kipengele kwa kipengele kwa sababu anajua haki zake na umeandika kwa lugha ambayo yeye anaifahamu vizuri [English].


"Angekuwa hana mkataba maana yake ni mchezaji huru na angeweza kuondoka kwenda klabu yoyote. Kama kuna klabu inamuhitaji ije mezani tuzungumze waweke mzigo tuwaachie mchezaji.


"Hao wanaosema wamemsajili Chama hawana huo uwezo, kwa hela yao ya ‘ndondondo si chururu’ hawana uwezo wa kumnunua Chama!


"Kama wanamtaka Chama wasubiri siku tukiachana nae kama ambavyo imewalazimu kusubiri miaka 13 kumchukua Jonas Mkude ndio hivyohivyo wavute subira.


"Na niwapongeze kwa kuwa na subira, walianza kumtamani Mkude miaka mingi sana na walifanya majaribio mengi lakini wakachemsha! Wakina Bin Kleb, Seif Magari, Yusuf Manji, Isack Chonjo, wote waligonga mwamba.


"Hatimaye wamekuja kutomiza ndoto yao ya kuwa na Mkude baada ya miaka 13, sisi tulipoamua kumuachia," amesema Ahmed.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post