Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa taarifa zinazosambaa kuwa beki wao raia wa Congo DR, Joyse Lomalisa Mutambala kuwa ameandika barua kuomba kuondoka klabuni hapo ni za uongo.
Kamwe amesema hayo wakati akizungumza na na Wasafi TV kufuatia mambo mbalimbali yanayoendelea katika klabu hiyo hususan masuala ya usajili wa wachezaji wapya.
"Hizo tetesi zinaanzishwa na watu wengine kwa makusudi, wakati huu wa usajili taarifa za uongo zinaenezwa kwa makusudi.
"Lomalisa ni mchezaji wa Yanga SC, bado anamkataba wa mwaka mmoja ataendelea kucheza Yanga na hajaomba kuondoka kama inavyoelezwa.
"Mchezaji akitaka kuondoka lazima afuate procedure, sisi tutamruhusu. Lakini Lomalisa hajaomba kuondoka," amesema Alikamwe.
Post a Comment