Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Mbeya City imetozwa faini ya Tsh laki tano (500,000) kwa kosa la watoto waokota mipira kuchelewa kwa makusudi kurejesha mipira kiwanjani kwenye mchezo wa sare ya 3-3 dhidi ya Yanga uwanja wa Sokoine.
Sambamba na hilo Mbeya City imetozwa faini Tsh milioni moja (1,000,000) kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa wachezaji wa Yanga wakati wakishangilia moja ya mabao waliyofunga.
Aidha klabu ya Yanga imetozwa faini ya Tsh milioni moja (1,000,000) kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa walinzi wa uwanjani kwenye mechi hiyo ambayo Yanga ililazimika kutoka nyuma 3-0 na kusawazisha magoli yote kunusuru alama moja kwenye sare ya 3-3.
Post a Comment