Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Yanga wako mkoani Mbeya ambapo jioni ya leo saa 10 watashuka uwanja wa Sokoine kumenyana na Mbeya City katika mchezo wa raundi ya 29 ligi kuu ya NBC
Tayari Wananchi wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo hivyo leo watakuwa na nafasi ya kupewa gwaride la heshima kutoka kwa Mbeya City
Gwaride kama hilo pia watalipata katika mchezo utakaofuata dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Ijumaa, Juni 09 siku ambayo watakabidhiwa taji lao la 29 ligi kuu
Shamrashamra za ubingwa zitaanza Mbeya na kuhitimishwa jijini Dar es salaam Juni 10 kabla ya Yanga kuelekea Tanga wanakokabiliwa na mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc
Mkufunzi wa Yanga Nasreddine Nabi leo huenda akawapa mapumziko baadhi ya wachezaji hasa wale waliotumika katika mchezo uliopita wa fainali kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger
Yanga inakabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi nne katika siku 9
Post a Comment