Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Imebainika kuwa Yanga wapo katika mazungumzo ya kumsajili winga raia wa Ivory Coast, Aubin Kramo Kouame ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Asec Mimosas ya nchini humo.
Kramo mwenye umri wa miaka 27 anatumia zaidi mguu wa kushoto, huku akiwa anamudu vyema kucheza winga zote za kulia na kushoto ambapo msimu uliopita alifanikiwa kuifungia timu hiyo mabao tisa na kutoa pasi nane za mabao.
Chanzo kutoka nchini Ivory Coast kimeliambia Championi Jumatatu, kuwa Yanga wapo mazungumzo ya kumsajili winga huyo ambaye ni moja kati ya wachezaji bora ndani ya Ligi ya Ivory Coast.
Pia chanzo hicho kimeongeza kuwa Yanga wamehitaji pia huduma ya mchezaji mwingine kutoka timu hiyo anayekipiga katika nafasi ya beki wa kulia huku pia mazungumzo yakiwa yanaendelea kwa pande zote mbili.
“Ni kweli Yanga wapo katika mazungumzo kwa ajili ya kumpata winga, Aubin Kramo ambaye amkuwa na misimu mizuri hapa Asec lakini sio huyo tu bali hata beki yule wa kulia, Kouassi Attohoula Yao pia Yanga wanamhitaji na wapo pia kwenye mazungumzo.
“Hakuna jambo ambalo limekamilika mpaka sasa kutoka kwa wachezaji wote hao wawili ila Yanga wapo katika mazungumzo nao ya kuwasjili kama wataafikiana na uongozi basi watasajiliwa,” kilisema chanzo hiko.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe akizungumza kuhusiana na usajili wa Yanga alisema kuwa: “Yanga kila msimu huwa inafanya usajili lakini usajili wa msimu ujao utakuwa usajili mzuri wenye manufaa kwa timu na sio kuwafurahisha watu.
“Hivyo wapenzi wa Yanga watulie kwani uongozi unafahamu nini unafanya,” alisema kiongozi huyo.
Post a Comment