Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Makamu wa Rais wa klabu ya Yanga Arafat Haji amesema mashabiki na Wanachama wa Yanga hawapaswi kuwa na wasiwasi baada ya kuondoka Kocha Nasreddine Nabi kwani viongozi wapo kazini kuwaandalia mazuri zaidi
Nabi ameondoka Yanga baada ya mkataba wake kumalizika akiwa amewatumikia Wananchi kwa misimu miwili na kuwapa mataji sita na fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat ameandika ujumbe huu;
"Wananchi wenzangu kwanza kabisa tumshukuru Kocha Nasreddine Nabi kwa kazi kubwa aliyoifanya tangu alipojiunga na klabu yetu hadi alipoondoka. Ametupa heshima kubwa sana, tumeshinda Ngao ya Jamii mara mbili, ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili, ubingwa wa Azam Sports Federation Cup mara mbili na kutufikisha Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kuja na kuondoka ni sehemu ya maisha ya soka, Nabi alikuja na sasa ameondoka kama ambavyo wamewahi kuja na kuondoka wachezaji, makocha na hata viongozi wengi. Nabi sio wa kwanza kuondoka na hatakuwa wa mwisho, watu wataendelea kuja Yanga na wakati wa kuondoka ukifika wataondoka.
Wananchi tunaomba tuendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki, viongozi wenu tupo kazini tunaomba mtuamini na mtupe muda kwa sababu mambo mazuri yanakuja msiwe na wasiwasi wala haraka.
Kama tuliweza kumpata Nabi ambaye ametufikisha hapa leo kwa nini tushindwe kupata Kocha atakaetutoa hapa na kutupeleka juu zaidi? Hakuna kisichowezekana, ni mipango tu na wenye Mipango bado tupo Sana!
Wananchi msiwe wanyonge, sisi ndio wafalme wa soka nchi hii!! Kwa mafanikio tuliyonayo makocha wengi wakubwa wa Afrika na nje ya Afrika wanatamani kufundisha Yanga.
Asante kwa kumbukumbu nzuri uliyotuachia Kocha @nabinasreddine , tunakutakia kila la kheri katika safari yako mpya. Karibu tena Tanzania, Jangwani ni nyumbani."
Post a Comment