Tulikubaliana nisaini miwili, Yanga wakaandika mitatu - Fei Toto

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' amedai kuwa alikubaliana na viongozi wa klabu hiyo kusaini mkataba wa miaka miwili lakini walimbadilishia na kumwandikia miaka mitatu kwa vile hajui lugha ya Kiingereza huku mkataba wakiuandika kwa lugha hiyo ya kigeni.


Fei Toto ambaye ana mgogoro na klabu yake hiyo, amesema hayo leo Alhamisi, Juni 1, 2023 wakati akihojiwa na Power Breakfast ya CloudsFM.


"Shida yangu #Yanga ni manyanyaso si mshahara, nilisaini mkataba wa miaka miwili kumbe yeye Kiongozi aliongeza mwaka mmoja bila ridhaa yangu, mkataba uliandikwa kwa Kiingereza.


"Nilikaa kwa Saa sita na Kiongozi wangu wa Yanga, alikuwa yeye na Makamu wake, nikamwambia waliyokuwa wakinitendea, akasema tusameheane, nikamwambia nimemsamehe lakini siwezi kubaki.


"Fedha ya usajili tulikubaliana Tsh milioni 100 kwa pamoja, pia si kweli walinipa fedha yote, nilipomaliza kusaini mkataba waliniingizia Tsh milioni 10 tofauti na tulivyokubaliana, ikaenda hivyo kupewa hela mpaka tugombane ndio wananipa kimafungu mafungu.


“Leo naomba niseme jambo ambalo mashabiki wa Yanga hawajui nimenyanyaswa sana Yanga. Mama Yangu ametukanwa, kama ningekuwa siipendi Yanga ningevunja mkataba kipindi kile hakuna mdhamini wakati ule inafika miezi 3 sijapewa mshahara," amesema Fei Toto.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post