Beki wa kati wa Azam FC Daniel Amoah ameongeza mkataba mwaka mmoja kuendelea kubakia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.
Klabu ya Singida Fountain Gate FC imemuongezea mkataba wa miaka mitatu kiungo wake, Aziz Andambwile utakaomalizika June 2026.
Klabu ya Simba SC ipo kwenye mazungumzo ya usajili na golikipa Caique Luiz Santos de Purificacao mwenye umri wa miaka 25 kutoka Ypiranga FC ya kwao Brazil
Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano na Mchezo Clatous Chama raia wa Zambia ya kumuongeza mkataba mpya wa miaka miwili.
Klabu ya Yanga huenda ikaachana na beki wao Mamadou Douambia raia wa Mali.
Baada ya kuachana na simba SC, aliyekuwa golikipa nambari mbili Beno David Kakolanya anatarajiwa kujiunga na Azam FC.
Mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Kibu Dennis amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo utakaomalizika June 2025
Klabu ya Singida Fountain Gate Fc ya Singida imethibitisha kumuongeza mkataba mpya wa miaka 2 kiungo wake Bruno Gomes Barroso raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 26, mkataba huo utakaomalizika juni 2025.
Klabu ya Singida Fountain Gate imemuongeza mkataba kiungo wake, Yusuph Kagoma utakaomfanya aendelee kusalia kwa walima alizeti hao wa hadi 2026.
Klabu ya Yanga imethibitisha kuachana na Abdallah Shaibu (Ninja)
Beki kulia, Nathanael Chilambo atasalia Azam FC hadi mwaka 2025, baada ya Kusaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Klabu ya Kitayosce FC (Tabora United) ipo kwenye mazungumzo na Mshambuliaji wa Yanga Crysin Ngushi ambaye mkataba wake umefikia tamati.
Klabu ya Dodoma Jiji Imekamilisha usajili wa wachezaji wawili, ambao ni kiungo Gustapha Simon na Winga Idd Kipagwile.
Klabu ya Coastal Union imethibitisha kuachana na wachezaji wake wawili ambao ni Yusuph Athuman pamoja na Yusuph Jamali Kisongo.
Klabu ya Namungo imethibitisha kuachana na wachezaji 7, ambao Chareli, Bressing, Smith, Farjala, Yangson, Bwenzi na Abdulrazack.
Klabu ya Simba tayari imetuma ofa ya kutaka kumsajili winga wa kimataifa wa Uganda na Vipers SC, Milton Karisa mwenye umri wa miaka 27.
Klabu ya Namungo FC ya Ruangwa Mkoani Lindi imetaganza kumsajili beki Erasto Edward Nyoni kutoka klabu ya Simba SC.
Klabu ya Azan Fc imethibitisha kumuongeza mkataba mpya kiungo wao James Akaminko utakaomalizika juni 2026.
Mshambuliaji wa Azam Fc Prince Dube amesaini mkataba mpya wa miaka 3 wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi juni 2026.
Klabu ya Azam FC imethibitisha kumuongeza mkataba mpya wa miaka 3 Sospeter Bajana utakaomfanya aendelee kusalia katika viunga vya Azam Fc hadi mwaka 2026.
Uongozi wa Klabu ya Yanga sc umepanga kumuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja winga wao Jesus Moloko
Danny Lyanga, D. Okoyo, Tariq Seif na Ismail Aziz wote wamejiunga na Klabu ya JKT Tanzania iliyopanda daraja msimu huu wa 2023/2024.
Cleophace Mkandala amejiunga na Kagera Sugar FC ya Kagera akitokea Azam FC.
Uongozi wa Klabu ya KMC upo kwenye mazungumzo na kocha wao mkuu Jamhuri Kiwelu ili kumuongeza mkataba mpya baada ya aliokuwa amesaini kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
KMC pia ipo kwenye mazungumzo na beki wa pembeni wa Yanga, David Brayson baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.
Klabu ya Yanga sc imethibitisha kuachana na nyota wao Dickson Ambundo na Benard Morrison.
Klabu ya Coastal Union imethibitisha kuachana na nyota wao raia wa Uganda Joseph Zziwa pamoja na beki wao wa pembeni Emery Nimubona raia wa Burundi pia Coastal Union imeachana na golikipa wao Mahmoud mroville raia wa Comoro
Klabu ya simba imethibitisha kuachana na kiungo wao Victor Akpan raia wa Nigeria, Simba pia imeachana na golikipa Beno Kakolanya, wengine ambao Simba imeachana nao ni Jonas Mkude, Mohamed Quatara, Erasto Nyoni na Nelson Okwa,
Klabu ya Coastal Union imethibitisha kuachana na wachezaji wao wawili ambao ni Djibril Naim Olatoudji pamoja na Geurold Mwamba wa Mwamba
Uongozi wa Klabu ya Yanga sc umepanga kumuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja winga wao Jesus Moloko.
Simba pia ipo kwenye mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya kiungo wake Sadio Kanoute raia wa Mali mwenye umri wa miaka 26.
Klabu ya Azam FC ipo kwenye mpango wa kumsajili beki wa kushoto, Joyce Lomalisa kutoka Yanga SC.
Uwezekano wa beki wa Kati kutoka Kenya, Joash Onyango kusalia Msimbazi msimu ujao wa 2023/24 unazidi kuwa mdogo baada ya beki huyo kuendelea na Msimamo wake wa kutaka kuondoka Klabuni hapo.
Klabu ya JKT Tanzania ipo kwenye mazungumzo na Tariq Seif Kiakala Kutoka Mbeya City pamoja na Deusdedity Cosmas Okoyo kutoka Geita Gold FC.
Vilabu vya Dodoma Jiji, Namungo FC na JKT Tanzania vinahaha kuinasa saini ya Mshambuliaji wa Geita Gold, Dany Lyanga
Majina yana Philippe Kinzumbi kutoka TP Mazembe pamoja na Aubin Kouame Kramo kutoka ASEC Mimosas ni Miongoni mwa majina yaliyopo kwenye orodha ya Wachezaji watakaosajiliwa na Yanga sc msimu ujao wa 2023/204.
Baada ya kuachana na klabu ya Azam FC Ismail Aziz Kada huenda akajiunga na JKT Tanzania iliyopanda Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2023/24 kwa mkataba wa miaka 2.
Uongozi wa Klabu ya Simba upo Kwenye Mazungumzo na TP Mazembe ili kumsajili Mshambuliaji wao, Jean Balake moja kwa moja ambaye amebakiza mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.
Klabu ya Simba SC, imekamilisha usajili wa Winga Leandre Essomba Willy Onana raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka kutoka Rayon Sports ya Rwanda kwa mkataba wa miaka miwili.
Simba pia imefanikiwa kumresha Adel Zrane ambaye ni fitness Coach akichukuwa nafasi ya Kelvin Mandla aliyeana na Simba hivi Karibuni.
Klabu ya Azam FC kwenye hatua za mwisho kukamilisha Usajili wa beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Senegal na Teungueth, Cheikh Sidibe mwenye umri wa miaka 24, ili kuziba pengo la Bruce Kangwa ambaye huenda akaachwa
Klabu ya Azam FC, imekamilisha usajili wa Kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei toto’ kutoka Young Africans kwa mkataba wa miaka mitatu (3).
Klabu ya Simba imetajwa kupeleka ofa ya kuhitaji saini ya Mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Makabi Lilepo kwa mkopo na golikipa Issa Fofana kwa mkataba wa moja kwa moja.
Baada ya kuvunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma raia wa DR Congo anatajiwa kuitumikia Young Africans msimu ujao wa 2023/2024.
Usajili wa Willy Esomba Onana kwenda Simba SC kutoka Rayon Sports na Coulibaly Wanlo kutoka ASEC Mimosas upo Katika hatua za mwisho.
Klabu ya Azam FC ipo kwenye mpango wa kuhakikisha wanainasa saini ya Mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Lamine Jarjou mwenye umri wa miaka 21 raia wa Gambia kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Klabu ya Azam FC inatajiwa kuachana na Wachezaji Yahya Zayd, Cleophace Mkandala, Bruce Kangwa, Ismail Aziz Kada na Wilbol Maseke Changarawe.
Dickson Ambundo huenda akarejea Dodoma Jiji FC baada ya mkataba wake na Young Africans kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa 2022/2023.
Klabu hiyo ya Jijini Dodoma huenda ikaachana na Beki wa Kulia Hassan Kessy na Aman Kyata mwishoni mwa msimu huu wa 2022/2023.
Hassan Maulid Machezo Simba SCKlabu ya Simba imetajwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha Usajili wa kiungo Hassan Maulid Machezo kutoka Mbeya City, kwaajili ya kuziba pengo la Jonas Mkude, ambaye inadaiwa Simba wana mpango wa kuachana naye mwisho wa msimu huu wa 2023/2024.
Kuna uwezekano makubwa wa Yusufu Kagoma kuondoka Singida BS mwishoni nwa msimu huu na nafasi yake kuchukuliwa na Jonas Mkude kutoka Simba SC.
Klabu ya Simba inatajwa kuiwinda saini ya beki wa kati, Coulibaly Wanlo mwenye umri wa miaka 31 kutoka ASEC Mimosas ya kwao Ivory Coast.
Simba pia inaiwinda saini ya winga, Aubin Kramo Kouamé mwenye umri wa miaka 27 kutoka ASES Mimosas ya Kwao Ivory Coast pia.
Klabu ya Simba imetajwa kuwa kwenye mazungumzo na Winga Leandre Willy Essomba Onana mwenye umri wa miaka 23 kutoka Rayon Sports ya kwao Rwanda.
Onana ndiye Kinara wa Ufungaji katika Ligi Kuu ya Rwanda (Rwanda Premier League) akiwa na magoli 15 na assist 10.
Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wao, Hassan Saleh Dilunga kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mwingine.
Klabu ya Young Africans SC, ipo kwenye Mazungumzo ya kumsajili Mshambuliaji Khanyisa Mayo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Cape Town City ya Afrika Kusini.
Mayo ndiye Kinara wa Ufungaji Ligi Kuu ya Afrika Kusini (South African Premier Division), akifunga mabao 12 sawa na Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns.
Young Africans pia inahusishwa na Mshambuliaji wa Marumo Gallants, Ranga Chivaviro mwenye umri wa miaka 30.
Chivaviro ndiye Kinara wa Ufungaji kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, akiwa na magoli matano (5) sawa na Fiston Mayele wa Yanga SC, huku kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini (South African Premier Division), akiwa na magoli 9 kwenye michezo 17.
Klabu ya Simba SC inamnyatia kiungo mkabaji mahiri, Gatoch Panom Yiech raia wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 28 KutokaSt. George SC ya kwao Ethiopia.
Mkataba wa Yiech Panom Gatoch na St. George SC unatajiwa kufikia tamati June 30, 2023.
Kocha, Fred Felix Minziro huenda akajiunga na Mbeya City kama Kocha wao Mkuu kuanzia msimu ujao wa 2023/2024 akitokea Geita Gold FC.
Klabu ya Singida Big Stars FC imepanga kuachana na wachezaji watatu ambao ni beki wa kati Pascal Wawa, Yassin Mustapha na Mshambuliaji Hamis Tambwe mwishoni mwa msimu huu wa 2022/2023.
Mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City, Paul Nonga anatarajiwa kuacha kucheza rasmi soka la ushindani mwishoni mwa msimu huu wa 2022/2023.
Baada ya kustafu mpira wa miguu mchezaji huyo atakabidhiwa timu ya vijana ya Mbeya City kama kocha Mkuu.
Vilabu vya Dodoma Jiji, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar vimeonesha nia ya kutaka saini ya nyota Gustapha Saimon kutoka Coastal Union FC.
Beki wa Simba, Gadiel Michael na Mshambuliaji Habibu Kyombo wapo Katika hatua za mwisho kutua Singida Big Stars ya Mkoani Singida.
Young Africans pia ina mpango wa kuachana na winga wao Tuisila Rossien Kisinda mwenye umri wa miaka 23 kutoka DR Congo mwishoni mwa msimu huu.
Wachezaji wengine ambao Young Africans ina mpango wa kuachana nao kuelekea msimu ujao wa 2023/2024 ni Benard Morrison mwenye umri wa miaka 29, David Bryson, Crysin Ngushi, Dickson Ambundo na golikipa Eric Johora.
Beki wa Kimataifa wa Kenya, Joash Onyango mwenye umri wa miaka 30 ametajwa kuwasilisha barua ya maombi ya kuomba kuondoka katika klabu hiyo aliyoitumikia takribani miaka mitatu.
KLABU ya Singida Big Stars inaidaiwa kukamilisha usajili wa beki wa kulia Nicolas Wadada kutoka Ihefu SC.
Huo utakuwa usajili wa pili wa Singida Big Stars baada ya kukamilisha usajili wa beki Yahya Mbegu kutoka Ihefu SC, ambaye alikuwa kwenye rada za Simba SC.
Uongozi wa klabu ya Young Africans upo kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka mitatu (3) golikipa wao Metacha Mnata, baada ya mkataba wa mkopo wa miezi 6 kutoka Singida Big Stars kuisha mwishoni mwa msimu huu.
Wachezaji wengine ambao Young Africans inajadiliana nao kwaajili ya kuongeza mkataba mpya ni Jesus Moloko na Denis Nkane.
Beki wa kati wa Klabu ya Young Africans, Ibrahim Abdallah Hamad amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuwatumikia wananchi kwa miaka mitatu ijayo.
Klabu ya Simba SC ipo kwenye mazungumzo na kinda wa Geita Gold FC, Edmund John mwenye umri wa miaka 20.
Imeelezwa kuwa Klabu ya Simba ina mpango wa kuachana na Wachezaji wake 11 kuelekea msimu mpya wa 2023/2024.
Wachezaji hao waliotajwa ni Nelson Okwa na Patrick Victor Akpan wote kutoka Nigeria, Augustine Okrah kutoka Ghana, na Mohamed Ouattara kutoka Ivory Coast
Wengine ni Hamed Ismael Sawadogo kutoka Burkina Faso, Peter Banda Kutoka Malawi, Jimmyson Mwanuke, Nassoro Kapama, Beno David Kakolanya, Jonas Gerald Mkude na Gadiel Michael Kamagi wote Watanzania.
Klabu ya Simba SC imetajwa kukamilisha Usajili wa beki wa kushoto Yahya Mbegu kutoka Ihefu SC ya Mbeya ili kuziba nafasi ya Gadiel Michael anayeachwa.
Klabu ya Simba SC ipo kwenye mpango wa kuwasajili viungo, Sospeter Bajana, anayemaliza mkataba wake na Azam msimu huu pamoja na Brno Gomez kutoka Singida Big Stars FC.
Wengine walio kwenye mpango wa Simba SC ni kipa Fabien Mutombola na Mshambuliaji Martin Kizza wote kutoka Vipers ya Uganda.
Klabu ya Singida Big Stars imetajwa kuwa katika hatua za mwisho kukamilisha Usajili wa kipa wa Simba SC, Beno Kakolanya, wengine ambao Singida inatajwa kuwinda saini zao ni Benard Morrison kutoka Yanga SC.
Klabu ya Coastal Union ya Tanga ipo kwenye mazungumzo na kocha wao wa zamani, Juma Mgunda ya ili awe kocha wao ajaye kwa msimu ujao wa 2023/2024.
Golikipa nambari mbili wa Simba SC, Beno David Kakolanya amekataa ofa ya kwanza kutoka kwa timu ya kutaka kumuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye makazi yake Mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam.
Inaelezwa kiwa kipa huyo amepewa ofa ya mshahara wa milioni tano (5m) kwa mwezi pamoja na ada ya usajili milioni 60.
Kakolanya amekataa ofa hiyo na kutoa sababu kuwa anataka kwenda sehemu nyingine ili awe anapata nafasi ya kucheza.
klabu ya Singida Big Stars huenda ikaachana na beki wake wa pembeni, Yassin Mstafa mwishoni mwa msimu huu, kutokana na ufinyu wa nafasi ndani ya Kikosi hicho cha walima Alizeti.
Kuna uwezekano mkubwa wa beki wa pembeni wa klabu ya Ihefu SC, Yahaya Mbegu kujiunga na Singida BS msimu ujao wa 2003/2024.
Singida Big Stars pia ipo kwenye mazungumzo ya kumrudisha aliyekuwa Mshambuliaji wake, Habibu Kyombo endapo Klabu ya Simba itaamua kumuachia mwishoni mwa msimu huu.
Klabu ya Geita Gold ya mkoani Geita huenda ikaachana na Kocha wake Mkuu, Fred Felix Minziro kabla ya msimu huu kumalizika au mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa kutoka ndani ya viunga vya Geita Gold zinasema kuwa Uongozi wa klabu hiyo unafikilia kuachana na Minziro kwa sababu ya kutokuwa na maelewano na wasaidizi wake wa benchi la ufundi.
Klabu ya Simba imetajwa kumwania beki wa kati na Nahodha Msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda, Thierry Manzi mwenye umri wa miaka 26 kutoka AS Kigali ya kwao Rwanda.
Simba pia ipo kwenye Mazungumzo na Mshambuliaji Eric Benjamin Kabwe mwenye umri wa miaka 22 kutoka AS Vita Club ya kwao DR Congo.
Klabu ya Singida Big Stars ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili beki wa kulia wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Ibrahim Abraham.
Klabu ya Geita Gold ipo kwenye Mazungumzo ya kumuongezea Mkataba golikipa wao, Arakaza MacArthur raia wa Burundi baada ya kuridhishwa na kiwango chake.
Klabu ya Kitayosce FC ya mkoani Tabora, iliyopanda Ligi Kuu ipo kwenye hatua za mwishoni kukamilisha Usajili wa wachezaji wanne (4) kwaajili ya kusuka kikosi upya kuelekea msimu ujao wa 2023/2024.
Wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Kitayosce ni Washambuliaji Yacouba Sogne kutoka Ihefu SC, pamoja na Heritier Makambo ambaye hana timu, golikipa Wilbol Maseke Changarawe kutoka Azam FC na Beki Steven Duah kutoka Kagera Sugar.
Inaelezwa kuwa Mdhamini na Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ amemrejesha kwenye Bodi ya Simba aliyekuwa CEO wa zamani wa timu hiyo Crescentius Magori kwaajili ya kuongeza nguvu ya utendaji kazi ndani ya Bodi hiyo kuanzia Msimu ujao 2023/2024.
Wachezaji wanaoondoka Simba SC msimu ujao wa 2023/2024 ni pamoja na Ismail Sawadogo, Augustine Okrah, Gadiel Michael anaenda Singida Big Stars FC, Habibu Kiyombo anaenda Singida Big Stars FC, Jonas Mkude anaenda Singida Big Stars pia, mwingine ni Mohammed Outtara, huku Joash Onyango akiwa 50%/50%.
Klabu ya Coastal Union FC ya Tanga imeachana na golikipa wake Mahamoud Mroyvil pamoja na beki wake wa kulia Emery Nimubona raia wa Burundi.
Post a Comment