Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
KAZE - Wakati kocha wa Singida Big Stars, Hans Pluijm akitajwa kupewa mkono wa kwaheri, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ndiye anatajwa anaweza kurithi mikoba yake.
MKUDE - Kiungo mkongwe aliyeichezea Simba kwa miaka 11, Jonas Mkude huenda akajiunga na Singida Big Stars ama kubaki Msimbazi kutokana na mvutano wa viongozi uliopo kwa sasa.
KAMETA - Beki wa pembeni, David Kameta 'Duchu' anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC msimu ujao, wakati miamba hiyo ya Chamazi ikiwa 'bize' na kusafisha timu kwa ajili ya usajili mpya.
BRYSON - Tangu beki wa kushoto, David Byrson, ajiunge na Yanga 2021, hakuwahi kucheza kwa kiwango kikubwa, hivyo inasemekana ni kati ya wachezaji ambao panga linawahusu na huenda akarejea kwenye timu yake ya zamani, KMC.
MASEKE - Kipa aliyeachwa na Azam FC, Wibol Maseke huenda akwa sehemu ya kikosi cha KMC ama Geita Gold msimu ujao, kutokana na timu hizo kuonyesha nia ya kumsajili.
Post a Comment