Ten Hag aingia vitani kumsaka mbadala wa Maguire

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Beki wa Manchester United, Harry Maguire ataondoka katika dirisha lijalo la usajili la kiangazi baada ya mazungumzo na mabosi wake.


Beki huyo alisugua benchi chini ya kocha Erik ten Hag kutokana na kukosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza tangu ujio wa Lisandro Martinez aliyetokea Ajax.


Kwa mujibu wa mkali wa usajili Ulaya, Fabrizio Romano uongozi wa Man United unajiandaa kuachana na wachezaji zaidi ya saba Maguire akiwemo kwenye orodha. Wachezaji wengine ambao hawatakiwi katika kikosi cha msimu ujao ni Alex Telles, Eric Bailly, Wout Weghorst, Brandon Williams, Anthony Martial, cott McTominay, Fred, na Dean Henderson. Kwa upande wa Donny van Beek, inaelezwa anataka apewe muda wa kucheza, lakini ataangalia uwezekano wa kuondoka.


Wakati huohuo beki bora wa Serie A Msimu huu anayekipiga Napoli na timu ya taifa ya Korea Kusini, Kim Min-jae amewaaga wachezaji wenzake na inaripotiwa atajiunga na Man United dirisha hili la usajili. Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 na Man United ipo tayari kununua mkataba wake wenye thamani ya Pauni 42 milioni.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post