Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya shamra shamra za ubingwa wa ligi kuu hapo jana, kikosi cha Yanga leo kinaelekea mkoani Tanga kwaajili ya mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc.
Jumatatu Juni 12, fainali ya FA itapigwa katika uwanja wa Mkwakwani kuanzia saa 9:30 Alasiri.
Hili ni taji la tatu Yanga inawania msimu huu baada ya kushinda Ngao ya Jamii na ligi kuu ya NBC.
Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema wataondoka Dar es Salaam Asubuhi kuelekea Tanga ambapo jioni watafanya mazoezi yao ya mwisho tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali.
Ratiba haijawa rafiki sana kwa Yanga lakini wachezaji wameendelea kupambana na kujitoa ili kutimiza malengo ya timu msimu huu.
Post a Comment