Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Muda wowote Yanga watatangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo wake mchezeshaji, Salum Aboubakari ‘Sure Boy’.
Kiungo huyo alijiunga na Yanga katika msimu uliopita akitokea Azam FC ambayo ilivunja naye mkataba.
Yanga imepanga kuiboresha safu hiyo ya kiungo kwa ajili ya msimu ujao ambao wanakwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa ambazo tumezipata, Yanga wamefikia makubaliano ya kumuongezea mkataba huo baada ya makubaliano ya pande mbili kati ya mchezaji na uongozi wa Yanga.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa katika mkataba huo baadhi ya vipengele vimeboreshwa ikiwemo mshahara ambao umeongezeka mara mbili zaidi aliokuwa anaupata awali.
Aliongeza kuwa uongozi unaendelea kuboreshewa mikataba ya wachezaji ambao inamalizika katika msimu huu.
“Sure Boy tayari ameongeza mkataba wa kuichezea Yanga, kilichobakia ni kutangazwa pekee kwa mashabiki. Ameongezewa mkataba huo kutokana na ubora ambao ameuonyesha katika msimu uliopita ikiwemo katika michuano ya kimataifa,” alisema mtoa taarifa huyo.
Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said alizungumzia hilo hivi karibuni la usajili kwa kusema kuwa: “Hakuna mchezaji yeyote atakayeondoka yule aliyepo katika mipango ya timu.”
Post a Comment