Simba Sc yaingia mkataba wa Sh bil 4 na Sandaland kutengeneza jezi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Club ya Simba imetangaza kuingia mkataba wa utengenezaji na usambazaji wa jezi na kampuni ya Sandaland The Only One, mkataba huo wa miaka miwili una thamani ya Tsh. Bilioni 4 ambapo ni sawa na Tsh Bilioni 2 kila mwaka, hiyo ikiwa ni ongezeko la 100% kutoka Tsh Bilioni 2 kwa miaka miwili zilizokuwa zinatolewa na Mdhamini wao aliyepita Vunja Bei.


Brand ya Simba imeendelea kupanda kwa thamani kwani mkataba wake wa uuzaji na usambazaji wa jezi umekuwa ukiongezeka kwa kiwango kikubwa kila mwaka.


Miaka mitano iliyopita Simba SC ilikuwa inapata Tsh. milioni 100 kwa mwaka kutoka UHL Sport, 2019 ikawa inapata Tsh milioni 300 kutoka UHL Sport, 2020-2022 Simba SC ikawa inapata Tsh Bilioni 1 kwa mwaka kutoka Vunja Bei na sasa ni Tsh Bilioni 2 kwa mwaka kutoka Sandaland The Only One.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salim Abdallah Muhene “Try Again” akiongea kwenye usiku wa kubwa zaidi Jijini Dar es salam leo, amesema “Nampongeza Sandaland kwa kupata nafasi hii, alijaribu mara ya kwanza hakufanikiwa lakini muda huu amepata, namshukuru pia VunjaBei kwa udhamini aliotupatia.”

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post