Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Refa wa ligi kuu ya Uingereza Antony Taylor alivamiwa na mshabiki wa timu ya Roma alipokuwa akipelekwa katika uwanja wa ndege wa Budapest.
Katika video zanazosambaa mitandaoni Taylor alionekana akivamiwa pamoja na familia yake wakirushiwa chupa na viti na kikundi hicho kilichokuwa kimejaa hamaki.
Muungano wa marefa wa soka wa kulipwa la Uingereza(PGMOL) katika taarifa ulisema kuwa lunafahamu tukio hilo na kulaani vikali shambulizi hilo kwa mwenzao.
"Tumeshangazwa na unyanyasaji usio na msingi wa kuchukiza uliokelezwa kwa Antony Taylor na familia yake alipokuwa akirejea nyumbani baada ya kuchezesha fainali ya Europa," taarifa hiyo ilisoma.
Muungano uliahidi kusimama naye Taylor licha ya mashambulizi anayopokea mitandaoni kutokana na maamuzi yake uwanjani.
Klabu ya Sevilla iliishinda Roma kupitia mikwaju ya penalti huku wakimkabidhi meneja Jose Mourinho kichapo cha kwanza katika fainali za michuano ya bara Uropa.
Taylor aliwaonyesha wachezaji 14 kadi ya manjano katika fainali hiyo, kadi nyingi zaidi kuwahi kuonyeshwa kwa mechi yoyote.
Mechi hio pia ilichezwa dakika thelathini katika kipindi cha ziada baada ya kuambulia sare ya bao moja.
Baada ya mechi hiyo video zilienea mitandaoni Jose Mourinho akimfokea na Kumtusi Taylor katika eneo la Kuegesha magari.
Mourinho alihisi muamuzi huyo aliipendelea timu ya Sevilla kushinda mechi hiyo baada ya Taylor kukosa kuwapa penalti baada ya mpira kumgonga mkono mchezaji wa Sevilla ndani ya sanduku.
Uefa ilisema inasubiri ripoti ya waamuzi kuhusu mechi hiyo kabla ya kumchukulia hatua yoyote Mourinho.
Chanzo: Radio Jambo
Post a Comment