Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kufuatia wimbi la Wachezaji kutoka Ulaya kutimkia Saudi Arabia wakiwemo Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, N'golo Kante, Ruben Neves na Kalidou Koulibaly ambaye yupo mbioni, Rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya, (UEFA) Aleksander Ceferin ana maoni tofauti kuhusu hatua hiyo ya timu kutoka Saudia.
Cerefin (55) raia wa Slovenia amesema hatua hiyo ni makosa makubwa kwenye soka Saudi Arabia kwani walipaswa kuwekeza kwenye soka la vijana kuliko kutumia fedha nyingi kuwasajili wachezaji ambao wanakaribia kumaliza soka lao.
Akijibu swali kuhusu mradi wa Saudia unaotishia UEFA, Ceferin amesema: "Kununua wachezaji wanaomalizia soka lao sio mfumo wa kuendeleza soka, kosa kama hilo walilifanya China. Wanapaswa kuwekeza kwenye soka la vijana, walete makocha, na waendeleze wachezaji wao wenyewe”
Post a Comment