Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kiwango waliochoonesha Yanga katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kimeachwa wengi midomo wazi.
Kiwango cha Yanga kimeshtua wengi na hivyo wataiweka nchi katika Timu zinazoogopwa Michuano ya Kimataifa.
Akizungumza Karia amesema;
“Mheshimiwa Rais Timu Hii imetupa Heshima kubwa sana na imetupa na deni, ushindi wa Yanga tunaufurahia lakini tujue kwenye mchezo wa Afcon utakuwa mgumu Waalgeria hawatatuchukulia poa.
“Timu zetu nne zitakazoshiririki kwenye michuano ya CAF msimu ujao utaziita tena hapa Ikulu na utaziita kwa ajili ya Kombe,” Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia
Post a Comment