Rais Samia aingilia kati sakata la Fei Toto, atoa maagizo haya

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wakati sakata la Kiungo wa Yanga Feisal Salum kutaka kuvunja Mkataba na Klabu ya Yanga likizidi kupamba moto huku mchezaji huyo akijiandaa kufungua shauri CAS.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni kama anakwenda kulimaliza suala hilo baada ya kuuomba uongozi wa Yanga kukaa chini na mchezaji huyo na kumaliza tofauti zao.


Akizungumza katika hafla ya kuipongeza Klabu ya Yanga, Ikulu Jijini Da es Salaam Rais Samia amesema;


"Viongozi wa Yanga nina ombi kwenu, sifurahii kusikia mnakuwa na mizozo na Wachezaji na sitaki kusema mengi nataka niwaambie tu hii ishu ya Feitoto hebu kaimalizeni, kaimalizeni ili tuangalie mbele sasa haipendezi Club kubwa kama hii nzuri iliyofanya kazi nzuri mnakuwa na kaugomvi na katoto.... hebu kamalizeni muende vizuri, nitasubiri kupata mrejesho wa hii siku yoyote mkiwa tayari karibuni nyumbani mje kunipa mrejesho"

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post